Taarifa ya Pamoja 2022

Kuanzia tarehe 15 mwezi wa nane hadi tarehe 15 mwezi wa tisa mwaka 2022, wanafunzi 10 kutoka chuo kikuu cha Dar es saaam (UDSM) na wanafunzi 10 kutoka chuo kikuu cha Münster Westfalische Wilhelms Universität (WWU) walifanikisha awamu ya kwanza ya mabadilishano ya kitamaduni kati ya vyuo hivyo.

Picha ya pamoja mbele ya International Office

Programu hii ilifanikiwa chini ya “Pamoja – Tanzania German Exchange Project”, program hii ilijikita katika kuutana na kujifunza tamaduni za pande mbili za program hii yaani Tanzania na Ujerumani. Wananfunzi 10 kutoka chuo kikuu cha Muenster wanamekua wakikutana tangu mwanzoni mwa majira ya joto (kiangazi) mwaka 2021 kuandaa program hi na vitu vitakavyofanyika katika program ya Pamoja. Maandalizi yalihusu bajeti ya fedha, maswala ya kiuongozi ambayo inajumuhisha maombi ya viza na hati zote muhimu pamoja na mahudhui yanayohusiano ya mtihani kuhusu Tanzania baada ya ukoloni wa wajerumani, historia ya ujerumani, jiografia na historia ya Tanzania, pamoja na taarifa ya mtihani wa mataifa ya kusini unaohusisha maswala ya ubaguzi wa rangi.
Baada ya maandalizi kukamilika awamu ya kwaza ya program ilifanyika kati ya katikati ya mwezi wa nane hadi katikati ya mwezi wa tisa mwaka 2022. Wanafunzi kutoka UDSM na WWU walimaliza program hii nchini Tanzania. Programu ya wote ilihusisha kutembelea maeneo mbalimbali kama vile kujua kuhusiana na Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na maeneo ya karibu na chuo, kutembelea ubalozi wa Ujerumani Tanzania na shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na idadi ya watu duniani (UNFPA) pamoja na mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za mauaji ya kimbali ya nchini Rwanda (IRMTC) ambayo makao makuu yake yapo Arusha, vilevile wanafunzi wa Ujerumani waliweza kutembelea na kujua familia za wanafunzi kutoka Tanzania kutokana na makazi ya muda waliyopewa na familia za wanafunzi kutoka Tanzania.

Kupika ni kubadilishana kitamaduni kwa njia ya vitendo sana

Wanafunzi kutoka Muenster waliweza kujua na kuelewa kiundani kuhusu maswala ya kisiasa, kijamii na kidini. Vilevile maisha mfumo wa maisha baada ya ukoloni katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, kwa mantiki hiyo waliweza kujua maeneo mbalimbali yanayoozunguka hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro. Vilevile wanafunzi waliweza kujifunza kuhusu maeneo mbalimbalia ambayo yalikua kitovu cha biashara ya utumwa Afrika mashariki, hii ndio sababu wanafunzi 20 waliweza kutembelea visiwa vya Zanzibar na kuweza kujua hasa kuhusu mji mkongwe wa “Stone Town”.

Kuanzia mwezi wa nane hadi wa tisa mwaka huu wa 2023, wanafunzi wa kutoka Tanzania watasafiri kuelekea Ujerumani. Maandalizi ya awamu ii ya pili yanahusisha upande wa wanafunzi wa Tanzania na vilevie wa Ujerumani kama vile kufanya maombi ya viza ya Ujerumani (Schengen Visa), maandalizi ya hati muhimu, kupanga na kuhitimisha bima muhimu ikiwemo bima ya afya na maombi ya fedha za kufanikisha awamu ya pili ya programu, Vilevile kupanga mahudhui ya programu ya awamu ya pili namna itakavyokuwa.

Wikingerschach
Arusha National Park